JE, NIMONIA NI NINI NA HUSABABISHWA NA NINI?

Nimonia ni maambukizi kwenye mapafu ya mtu mtiza au motto, aghalabu yasababishwayo na bakteria au virusi. Ni hali ambayo hukinzana na hatimaye kuathiri mfumo wa kupumua.

Mar 19, 2024 - 19:22
Mar 19, 2024 - 19:26
 0  29
JE, NIMONIA NI NINI NA HUSABABISHWA NA NINI?
photo courtesy

Kutokana na makala yalichapishwa 12 Novemba 2022, na Shirika la habari la BBC Swahili, na kuboreshwa 29 Januari 2024; Nimonia ni maambukizi kwenye mapafu ya mtu mtiza au motto, aghalabu yasababishwayo na bakteria au virusi. Ni hali ambayo hukinzana na hatimaye kuathiri mfumo wa kupumua.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, (WHO), Watoto 740,000 chini ya miaka mitano waliiaga dunia kutokana na homa hiyo ya mapafu mnamo mwaka 2019. Ikumbukwe kuwa, Novemba 12 kila mwaka, ulimwengu huadhimisha "Siku ya kimataifa ya kupambana na Nimonia".

Wa hivi punde kuiaga dunia kutokana na Nimonia ni mwanahabari gwiji wa shirika la habari la NTV, Rita Tiniina. Hayo ni kwa mujibu wa matokeo ya upasuaji uliofanywa na Dkt. Peter Ndewa na Dkt. Michaka wa Serikali na Familia mtawalia.

 Swali: Nimonia ugonjwa gani? Je, unasambazwa au kuambukizwa kivipi? Kuna tiba?

Picha: GETTY Images

Nimonia au homa ya mapafu ni nini haswa?

Kwa lugha nyororo, Nimonia ni maambukizi yanayoshambulia mfumo wa kupumua. Tulivyotaja hapo awali, ni maambukizi yanayotokana na virusi, bakteria au hata kuvu.

Maambukizi yakitokana na bakteria, huzua hali ambapo maji na usaha hujikusanya katika eneo linalofanya kazi kuchuja hewa ya okisjeni na carbon dioxide wakati tunapopumua.

Hivyo basi, huwa vigumu mtu kupumua, hatua inayochangia  kupungua kwa kiwango cha okisjeni kupungua katika damu mwilini. Kiwango cha Okisjeni kikipungua kwa kiasi kikubwa husabaisha kifo cha cha yule aloathirika.

 

Dalili za Nimonia ni zipi?

Nimonia haibagui jinsia, ukwasi au ufukara, umri au cheo. Mtu yoyote anaweza kuugua homa ya mapafu. Dalili zake ni pamoja na

• Kupatwa ugumu wa kupumua

• Kuongozeka kwa mapigo ya moyo kwa dakika, kutokana na ugumu wa kupumua

• Joto kuongezeka mwilini ghafla

• Kutetemeka, kutokwa na jasho mwilini

• Kukohoa

• Maumivu kwenye kifua

• Kuumwa na kichwa, kuhisi kutapika,au kutapika, kuharisha

Haimaanishi kuwa kila baaya ya dalili zilizotajwa hapo juu kujidhihirisha, mtu anaugua Nimonia, la hasha. Himizo ni kwamba, kautafute ushauri wa mtaalamu wa kiafya pindi unapokumbana na mojawapo au dalili hizi kwa ujumla wake, ambapo utafanyiwa utafiti katika maabara na upewe matibabu. Shirika la afya duniani; WHO linasema kwamba iwapo maambukizi yametokana na bakteria au virusi madhara yake yako sawa. Hata hivyo dalili hutofautiana kidogo.

Iwapo homa hiyo imetokana na maambukizi ya virusi basi baadhi ya dalili anazokuwa nazo mgonjwa ni pamoja na kikohozi, joto mwilini, mafua na kupata matatizo ya kupumua.

            

PICHA: Fitopardo/Getty Images

 

Vipi unaweza kutambua mtoto anaugua homa ya mapafu?

 

Joto jingi mwilini

Watoto wanaweza kupata joto mwilini kwa sababu tofuati. Mara nyingi joto mwilini hutokea wakati mwili unapambana na ugonjwa. Lakini iwapo joto ni jingi sana au halishuki hata unapompatia mtoto dawa, unashauriwa umfikishe mtoto kwa daktari ili apate kuchunguzwa . 

 

Matatizo ya kupumua

wanavyopumua watoto huwa tofuati kila saa mchana. Wao hupata matatizo ya kupumua mara moja wanapopata maambukizi ya homa ya mapafu. Baadhi hutoa sauti kama firimbi kuashiria ugumu wanaopitia wakipumua. Hapa mzazi unashauriwa kuwa na uangalifu wa hali ya juu.

 

Uchofu

Ni vema utambue kuwa, mapafu hujaa maji kutokana na homa hii. Na ndicho kiini haswa kinachosababisha shida ya kupumua. Mtoto anahisi kuchoka. Iwapo mtoto wako anaonekana kuchoka saa zote, basi ni muhimu uusake ushauri wa daktari haraka iwezekanavyo.

 

Je homa ya mapafu inatibiwa vipi?

Ni muhimu kuzitambua dalili na mapema, baadhi yazo tumeziorodhesha hapo juu

Ikumbukwe kuwa, rahisi kutambua homa ya mapafu kwa watoto walio chini ya miaka mitano. Anapopata matatizo ya kupumua ni muhimu kumfikisha hospitalini haraka iwezekanavyo.

Virusi ndani ya mapafu vinaweza kuchukua siku kadhaa hadi wiki kusambaa mwilini.

Maambukizi ya bakteria yanaweza kutibiwa kwa dawa za Viuavijasumu au antibiotics. Ni muhimu kila mara kufanyiwa uchunguzi kwenye maabara ili kuhakiki ni ugonjwa upi unatibu, kabla ya hata kununua viuavijasumu kwenye apoteket (Pharmacy)

Hata hivyo iwapo maambukizi ni makali huenda mgonjwa akahitaji kulazwa hospitalini.

Wataalamu wanashauri kwamba wagonjwa wanaweza kupoa haraka kwa kuchukua hatua kama vile kupumzika na kunywa maji mengi.

 

Tafadhali pata ushauri wa ntaalamu wa kiafya pindi unapojihisi kuwa dalili zozote zinazokinzana na hali ya kawaida.

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow